KIPA chaguo la tatu wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga Ally Mustapha 'Barthez' amekanusha uvumi uliozagaa kwamba ana mipango ya kurejea klabu yake ya zamani ya Simba mara baada ya kumalizika mkataba wake katika kikosi hicho cha Yanga.
Barthez ameyasema hayo hivi karibuni mara baada ya kuwasili nchini na kikosi hicho kilichotokea nchini Misri ambapo ilikwenda kurudiana na mabingwa wa Afrika National Al Ahly ambapo Yanga ilitolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3.
Kipa huyo aliyepata kuwa tegemeo katika kikosi hicho msimu uliopita na kuipa ubingwa wa bara na Afrika mashariki na kati amedai bado ajatoa msimamo kuhusu hatma yake endapo mkataba wake utamalizika, ameongeza kuwa yeye ni mchezaji wa Yanga na mkataba wake ukiisha ataendelea kuwasikiliza Yanga kama watamuongezea mkataba mwingine ama vinginevyo.
Amesema ni ngumu kwa sasa kutangaza kurejea Simba kwani muda wa kufanya hivyo haujafika na ukifika atakuwa tayari kuzungumza, Barthez aliihama Simba misimu miwili iliyopita na kujiunga na Yanga, alipokwa namba na kipa wa kwanza wa sasa Deogratus Minishi Dida baada ya kuruhusu goli 3 ilipocheza na Simba.
Katika mchezo huo wa ligikuu ya bara mzunguko wa kwanza Yanga ilitoka sare na Simba ya kufungana mabao 3-3, lakini ilikuwa ikiongoza kwa magoli 3 hadi mapumziko, kipindi cha pili Barthez aliruhusu magoli matatu yaliyopelekea shutuma dhidi yake, tangia mechi hiyo Barthez ahajacheza katika kikosi cha kwanza.