Wachezaji
wa kikosi cha kwanza walihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu
katika kanisa la Cathedral mjini Barcelona na kutoa heshima zao za
mwisho kwa Vilanova, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 45
baada ya kusumbuliwa na maradhi saratani.
Mkewe
na watoto wao wawili wa kike pia walihudhuria pamoja na mtoto wao
kiume, Adria, anayechezea akademi ya Barca, na binti yake Carlota,
alilia sana.
Dani Alves (kushoto) na Neymar kulia
Lionel Messi alikuwepo pia kumuaga Vilanova
Pumzika kwa amani: Tito Vilanova amefariki akiwa kijana wa miaka 45
Ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji wa Barcelona, Lluis Martinez Sistach.
Marais
wa zamani wakiwemo Joan Laporta na Sandro Rosell walikuwepo kanisani,
pamoja na Wajumbe wa bodi walioongozwa na Rais wa sasa, Josep Maria
Bartomeu.
"Leo tunamuaga mpendwa wetu,"alisema Bartomeu. "Nakuahidi, daima atadumu katika mioyo yetu na hatutamsahau milele,"aliongeza.
Kwaheri: Gerardo Martino (kushoto) na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu pia walikuwepo
Waombolezaji mbalimbali wakiwa kanisani jana
Kipa wa Barca, Victor Valdes akiwasili na 'magongo' yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia