come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KAVUMBAGU. TWITE NI MALI YA YANGA- UONGOZI

Na Fikiri Salum

UONGOZI wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi na mshabiki wa timu yao kutokuwa na haraka wala kuumizwa vichwa na kauli zinazotolewa kuhusu wachezaji wawili wa kimataifa Didier Kavumbagu raia wa Burundi na Mbuyu Twite raia wa DRC Kongo na umesema wote hao ni mali ya Yanga na wataendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya viongozi wa Yanga ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao kwa madai kuwa wao si wasemaji, kiongozi mmoja wa Yanga amesema Kavumbagu na Twite wote wamemaliza mikataba yao lakini wataongezewa hivi punde.


'Kwa sasa Yanga iko katika maandalizi ya kufanya uchaguzi wake mkuu hivyo wachezaji wamepewa likizo fupi na kurejea makwao lakini wameshataarifiwa kuitwa muda wowote, na wale waliomaliza mikataba yao wameshaaelezwa kila kitu kuwa bado wanahitajika', alisema kiongozi huyo ambaye ni mjumbe.

Wachezaji waliomaliza mikataba yao ambao ni muhimu kuendelea kuichezea Yanga ni Mbuyu Twite, Didier Kavumbagu na Frank Domayo, aidha kipa Ally Mustapha 'barthez' ambaye amemaliza mkataba wa kuitumikia Yanga huenda akaongezewa mwingine kufuatia kocha wa timu Mholanzi Hans Van Der Pluijm kumuhitaji.

Pluijm aliwasilisha mapendekezo yake kwa uongozi kuwa Barthez anamuhitaji kutokana na uhodari wakle awapo golini,Kavumbagu hivi karibuni alikaririwa kuzitaka klabu zinazomuhitaji zijitokeze kufuatia Yanga kumchunia, lakini taarifa za ndani zinasema kuwa Kavumbagu alikuwa anatingisha kiberiti na tayari ameshawekwa mtu kati na viongozi wa klabu hiyo