|
|
Manuel Pellegrini alifyata mdomo kuhusu uwezekano
wa viungo wake Manchester City kutawazwa washindi wa ligi ya Premier
ingawa alishinikiza umuhimu wa kurejesha hatima yao mikononi mwao.
City walijipata kwenye usukani wa harakati za mguu niponye za kutwaa taji hilo baada ya kuandikisha ushindi wa 2-0 dhid ya Crystal Palace baada ya ninara wa ligi hiyo, Liverpool, kukomeshwa nyumbani kwa matokeo sawa na Chelsea ambao pia walijikita ndani ya kinyang’anyiro hicho.
“Faida kwetu? Hapana,” Pellegrini aliambia wanahabari, “Lakini inategemea na kile tutakacho tekeleza katika mechi zinazofuata.”
“Kwa sasa, tuko nafasi ile ile, Liverpool wana alama tatu mbele yetu na Chelsea moja. Kwa hivyo, hatuna budi kushinda mechi tatu tulizobaki.
“Ni muhimu kukosa kutegemea matokeo ya wengine. Liverpool hawakuwa na budi kushinda mechi moja na wamepoteza leo. La kheri ni kuwa hatima iko mikononi mwetu sasa.”
Meneja huyo mwananchi wa Chile anawania taji lake la kwanza Uingereza baada ya kujiunga na City mwanzoni mwa musimu huu na tayari amewaongoza kunyakua taji la League Cup.
Timu yake ambayo ina mechi moja ya ziada dhidi ya wapinzani wao wa karibu, itatawala ligi hiyo ikiwa watashinda mechi tatu zilizosalia kwani wana idadi kuu ya tofauti ya mabao ikilinganishwa na Liverpool na Chelsea.
Mwalimu huyo alisifu kikosi chake kwa kuonyesha utulivu na ukakamazu unaotakikana baada ya kukiri kwamba wachezaji wake walitizama kivumbi kati ya Chelsea na Liverpool kilichotangulia mechi yao.