come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ABDI BANDA KUSAINI MIAKA MIWILI YANGA

Uongozi wa Klabu ya Yanga uko katika hatua za mwisho za kumnasa beki wa Coastal Union na timu ya Taifa (Taifa Stars), Abdi Banda.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo, tayari beki huyo amekubali kuja kuichezea Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

"Tuko katika hatua za mwisho za kumnasa Banda, si unajua usajili siku hizi ni lazima ufuate taratibu zinazostahili," alisema mmoja wa viongozi wa juu wa Yanga.

Aliongeza kuwa Yanga itaendelea kufanya usajili wake kwa kufuata ripoti ya kiufundi ya kocha wao mkuu aliyeondoka Mholanzi, Hans van Pluijm.


Yanga ambao mwakani itashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho pia imetangaza kumrejesha kiungo wake, Omega Seme na huku ikimuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja beki Mbuyu Twite.

Hata hivyo, Yanga bado haijamuongezea mkataba kipa wake, Deogratius Munisi 'Dida" na Ally Mustapha 'Barthez' anayetajwa kurejea Simba.