Klabu ya Esperance ya Tunisia
imemfuta kazi kocha wake Ruud Krol kufuatia matokeo mabaya katika mechi
za makundi katika ligi ya vilabu bingwa ya Afrika.
Esperance ilianza mechi hizo kwa kuandikisha matokeo mabaya zaidi wikendi iliyopita baada ya kushindwa kwa mabao 2-1 na Entente Setif ya Algeria.
Timu hiyo baadae ilishindwa kwa mara ya pili mfululizo ilipofungwa mabao 3-2 na Al-Ahly Benghazi ya Libya, katika mechi iliyochezewa ugani Sfax Tunisia, kwa sababu za kiusalama.
Krol, ambaye amewahi kuwa nahodha wa Uholanzi katika kombe la dunia alikuwa amejiunga na Esperance mwezi Januari katika kandarasi ya miaka 3.
Wasaidizi wake vile vile wamefutwa kazi.
Esperance ndio timu yenye mafanikio zaidi katika historia ya ligi ya Tunisia.
Imewahi pia kushinda kombe la vilabu bingwa mara mbili.