WANAKWAMBIA adui yako mwombee njaa, Ndivyo unavyweza kutamka, mshambuliaji wa Yanga ambaye ameishia kukaa benchi kwa muda mrefu Jerry Tegete amefunguka na kuonyesha furaha yake kufuatia kuhama kwa mshambuliaji wa raia wa Burundi Didier Kavumbagu aliyesajiliwana mabingwa wapya wa soka Tanzania bara Azam fc.
Akizungumza na Staa wa Leo, Tegete amesema kuondoka kwa Kavumbagu hakutaweza kuiathili klabu yake ya Yanga kwa vile wana wachezaji mahiri ambao walikuwa hawatumiki sana na mwalimu, Tegete amedai kila mwalimu anayekuja Yanga amekuwa na falsafa yake ambapo hutumia wachezaji anaowahitaji.
Lakini kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja Yanga inao wengi na yeye ni miongoni mwao, 'Nimecheza mechi sita nimefunga magoli sita, hapo utaona uwezo wangu jinsi ulivyo kuwa mkubwa isipokuwa sijapata nafasi tu ya kuanza katika kikosi cha Hans Van Der Pluijm.
Uwezo wa Tegete umejidhihirisha katika mechi za mwishoni mwa msimu uliopita ambapo magoli yake yaliiwezesha Yanga kukimbizana na Azam ambao baadaye wakaja kuchukua ubingwa wa bara, Tegete alikuwa akimshutumu Kavumbagu kwa madai anamroga na ndio maana amekuwa akiumia mara kwa mara.