come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TIMU 16 KUCHEZA LIGI KUU MSIMU UJAO

Wakati Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitarajia kukutana kesho kujadili mambo mbalimbali ikiwamo ripoti ya Kamati ya Mashindano ya shirikisho hilo, imedaiwa kuwa kamati hiyo imependekeza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao iwe na timu 16.

Taarifa ambazo Staa wa leo imezipata kutoka ndani ya uongozi wa TFF zimedai kuwa kamati hiyo timu mbili tu (Rhino Rangers na Oljoro) zimependekezwa kutoshiriki ligi hiyo msimu ujao baada ya kuporomoka daraja huku Ashanti United, iliyoporomoka daraja pia kwa mujibu wa Kanuni za Ligi za TFF, na timu nyingine mbili zilizofanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza licha ya kushindwa kufuzu, zitapata fursa ya kukipiga Ligi Kuu.


Hata hivyo, Jamal Malinzi, Rais wa TFF, alisema jijini Dar es Salaam jana mchana kuwa mambo yote yatajadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kesho.

"Jumamosi (kesho) saa 8:00 mchana kutakuwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ambacho pamoja na mambo mengine kitajadili ripoti ya Kamati ya Mashindano kuhusu mambo mbalimbali ya uendeshaji wa ligi yetu," alisema Malinzi.