come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TFF YADAIWA KUIHUJUMU YANGA KUHUSU KAVUMBAGU

Na Fikiri Salum

KUFUATIA klabu ya Azam fc ambao ni mabingwa wa soka Tanzania bara msimu wa 2013/14 kuitingisha klabu ya Yanga kwa kuwasajili waliokuwa wachezaji wao Didier Kavumbagu na Frank Domayo, imebainika kuwa shirikisho la kandanda nchini TFF inahusika kwa namna moja kufanikisha usajili wa nyota hao Azam.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na viongozi wa Yanga jana, inaonyesha kuwa TFF imeifanyia hila Yanga na kufanikisha usajili huo kwa Azam fc ambao ni mabingwa wa bara.

Yanga inasema kuwa iliomba ufafanuzi mapema kwa shirikisho hilo la kandanda nchini juu ya kanuni mpya za usajili wa wachezaji wa kigeni ambapo awali ilifahamika kuwa kila klabu itaruhusiwa kusajili wachezaji watatu wa kigeni badala ya watano.


Lakini TFF ilishindwa kuwapa Yanga ufafanuzi na zaidi iliwataka Yanga wasubiri watapewa majibu, uongozi wa Yanga tayari ulishafanya mazungumzo na Kavumbagu pamoja na Mbuyu Twite na kuwataka wasubirie majibu kutoka TFF kama wataruhusiwa kusajili wachezaji watano au watatu.

Taarifa hiyo ya Yanga inasema endapo TFF ingewapa ufafanuzi mapema kama ni kusajili wachezaji watatu basi ingewapa kisogo nyota wake hao, na kama ingeruhusiwa watano ingewapa mikataba mapema.

Lakini kitendo cha TFF kukaa kimya muda wote kumewapa mwanya maadui zao Azam kumsainisha mshambuliaji wake wa kutumainiwa Didier Kavumbagu ambaye ni raia wa Burundi, kuhusu Domayo.

Uongozi wa Yanga umedai kuwa ni hila za TFF kutaka kuwaharibia mipango yao, tangia TFF iingie madarakani imekuwa ikiwafanyia hila Yanga kuanzia sakata la Emmanuel Okwi hadi sasa Domayo.

Yanga ilishakubaliana na Domayo kwamba watampa mkataba mwingine lakini wanashangaa mchezaji huyo kuingia mkataba na klabu ya Azam tena kwenye kambi ya timu ya taifa iliyopo jijini Mbeya