Meya wa mji mkuu wa Canada
Toronto, Rob Ford anayekumbwa na utata anatarajiwa kuacha kazi kwa muda
ili kupata usaidizi kwa tatizo lake la kutumia madawa ya kulevya.
Bwana Ford mwenye azma ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba amesimamishwa kazi baada ya kukiri kutumia dawa za kulevya wakati alipokuwa Meya.
Alikiri kutumia Cocaine mwaka jana.
Kukiri kwake kunafuatia miezi miezi kadhaa ya yeye kukana madai ya kutumia madawa hayo lakini polisi walitoa kanda iliyoonyesha meya huyo akitumia Cocaine mwaka jana.
Jarida la Sun mjini Toronto, linamnukuu Ford mwenye umri wa miaka 44, akisema kuwa yuko tayari kuacha kazi kupata usaidizi na hata kusitisha kampeini yake.
Aliambia jarida hilo kuwa anashawishiwa na watu kutupilia mbali azma yake ya kugombea nafasi ya meya.
Hata hivyo jarida hilo lilisema limepata kanda ya menya huyo akiwatusi wanasiasa wengine.
Pia kanda za video zimetolewa katika miezi ya hivi karibuni zikimuonyesha bwana Ford akitoa matusi, kuwakemea na kuwatishia wafanyakazi wake na kutumia Cocaine.
Pia Bwana Ford anatuhumiwa kwa kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi. Hata hivyo amekanusha madai hayo.