come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAN CITY YAMETIMIA,WABEBA NDOO ENGLAND

MANCHESTER imetwaa ubingwa wa England baada ya kuifunga mabao 2-0 West Ham United jioni ya jana Uwanja wa Etihad, hivyo kumaliza msimu na pointi 86, mbili zaidi ya Liverpool walioshika nafasu ya pili.
 
Mabao ya City yamefungwa na Samir Nasri dakika ya 39 na Nahodha Vincent Kompany dakika ya 49. Liverpool imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Newcastle United. Skrtel alijifunga dakika ya 20 kuipa Newcastle bao la kuongoza, lakini Daniel Agger akaisawazishia Liverpool dakika ya 63 kabla ya Daniel Sturridge kufunga la ushindi dakika ya 65.  
 
Chelsea imemaliza katika nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Cardiff City mabao yakw yakitiwa kimiani na Schurrle dakika ya 72 na Torres dakika ya 75, huku bao la wapinzani wao likifungwa na Bellamy dakika ya 15.
 
Arsenal imemaiza katika nafasi ya nne kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Norwich City, mabao ya Ramsey dakika ya 53 na Jenkinson dakika ya 62. Everton iliyoifunga 2-0 Hull City imemaliza katika nafasi ya tano, wakati Tottenham Hotspur imemaliza ya sita baada ya kuifunga 3-0 Aston Villa na Manchester United iliyotoa sare ya 1-1 na Southampton  imemaliza ya saba.

Kama ilivyo ada, bingwa na timu tatu za chini yake watacheza Ligi ya Mabingwa, wakati wa tano wa sita watakwenda Europa League.  

Samir Nasri akishangilia bao lake