come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YOUNG KILLER 'MSODOKI' AWAPA SOMO WASANII CHIPUKIZI.

Na Robert Michael

Rapper wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya na "Hiphop" ambae anatamba na wimbo wake wa "Miss superstar" amewatahadharisha wasanii chipukizi kuwa makini na kazi zao.

Msodoki akireport katika blog hii anasema kuwa kuna tabia ya wizi wa music style hasa kwa wasanii chipukizi.

Vilevile msodoki amewashauri wasanii wachanga kuwa waache tabia ya kutoa mistari yao na kuwapa wasanii waliopiga hatua za hapa na pale kwa kudai kuwa eti wanasahihishwa mistari yao.

Msodoki amedai kuwa pamoja na kupitia changamoto nyingi alikuwa makini sana na kazi zake ndio maana ameweza kupiga hatua za hapa na pale.


Rapper huyo ambaye maskani yake ni "Jijini mwanza" amewaeleza wasanii chipukizi kuwa waamini uwezo wao na wasiombe msaada wowote wa kurekebishwa mistari yao kwa wasanii waliopiga hatua kwani ndio njia pekee ya wasanii chipukizi kuibiwa music style yao.

Aidha msanii huyo amesema music hauwezi kuendele bila wasanii chipukizi hivyo basi chipukizi wasaidiwe na sio kuibiwa.