come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SUAREZ ATAMANI KUREJEA AJAX

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Luis Suarez amesema anatumaini siku moja atarejea klabu yake ya zamani ya Ajax.

Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uruguay, ambaye anatakiwa na Real Madrid mwishoni mwa msimu, amesema ana deni kubwa katika klabu hiyo ya Uholanzi iliyomuibua akiichezea kwa misimu mitatu na nusu, kushinda nayo taji la Eredivisie na kuifungia mabao 81 katika mechi 110 za ligi hiyo.


Suarez ambaye klabu yake Liverpool imepoteza matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu England, amesema: "Wakati wore nimekuwa nikisema sikh moja nitarudi Ajax. Hata kama mocha atakuwa hanitaki, nitakwenda. Kweli!'

Akizungumza na gazeti la Helden, Suarez alisema: "Ajax ilikuwa hatua muhimu katika maisha yangu. Mke wangu Sofia na mimi hutuambii kith kuhusu Amsterdam na aina ya maisha yake, heshima kutoka kwa kila mmoja,".

"Tulikuwa na maisha ya furaha na tungeishi huko kwa amani. Tulizunguka sana jiji la Amsterdam,"'

Suarez, ambaye alishinda tuzo za Mwanasoka Bora wa Chama cha wachezaji wa kulipwa na Waandishi wa Habari England, alisema: "Ajax ilikuwa ni kila kitu kwangu na nimejifunza mengi huko. Nawapa sifa Ajax kwa kunifundisha mimi kutumia miguu yote, lakini pia namna ya kucheza bila ya kuwa na mpira na jinsi ya kuwa mchezaji wa timu.

"Martin Jol (kocha wa zamani wa Ajax) alinipa mimi hali ya kujiamini kwa kiasi kikubwa. Nilipewa heshima nilipokabidhiwa unahodha wa timu na nilihisi majukumu,".