Aliyekuwa kaimu kocha na
Mchezaji wa Manchester United Ryan Giggs amekiri kuwa hakuwa tayari kwa
majukumu ya kazi kama kocha wa klabu hiyo ya Uingereza.
Giggs alichukua hatamu kama kaimu kocha mwisho wa msimu uliopita baada ya kocha David moyes Kutemwa kufuatia msururu wa matokeo duni tangu achukue hatamu Old Trafford.
Giggs aliyekuwa kocha katika mechi nne za mwisho alitwaa ushindi katika mechi 1 akashindwa moja na kisha akatoka sare katika mechi ya mwisho Manchester united ilipomaliza msimu katika nafasi ya 7 .
Giggs alistaafu kama mchezaji msimu uliopita baada ya kuiwakilisha Man united katika mechi 963 na kufunga mabao 168 .