come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAXIMO KUITAKATISHA YANGA, AANZA NA KAMBI JANGWANI

Kocha mpya wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo, amesema hatakuwa na maneno mengi ila vitendo vyake uwanjani ndivyo vitakavyoinyanyua timu hiyo na kurejesha heshima na makali yake ndani na nje ya nchi.


Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Maximo alisema kuwa anakifahamu kilichomfanya Yanga impe ajira hiyo hivyo hatawaangusha viongozi na wanachama waliompa jukumu la kuiongoza timu.

Maximo alisema kuwa akiwa Yanga atakuwa na programu za muda mrefu na mfupi na kupitia mikakati hiyo Yanga itapata mafanikio iliyokuwa inayahitaji.

"Sitakuwa mzungumzaji sana kama nilivyokuwa kocha wa timu ya taifa, sasa nimekuja tofauti na majukumu ya klabu yana mipaka...ila mambo yangu yataonekana uwanjani," alisema Maximo.

Mbrazil huyo aliongeza kuwa anaziheshimu klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara kwa sababu hutoa upinzani kwa timu kongwe kila wanapokutana na amefurahishwa kusikia sasa Azam na Mbeya City zimekuwa tishio kwenye ligi hiyo ya juu nchini.

"Najua Azam, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na timu mpya ya Mbeya City zinatoa ushindani katika ligi ila bado naiheshimu Simba ambao ndiyo wapinzani wa jadi wa Yanga," alieleza kocha huyo ambaye aliipeleka Taifa Stars katika fainali za Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zilizofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2009.

Katika kuimarisha kikosi cha Yanga, Maximo amekuja na msaidizi wake kutoka Brazil na mshambuliaji mpya wa kimataifa.

Mtihani wa kwanza wa Maximo utakuwa katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) yatakayofanyika kuanzia Agosti 9 hadi 23 jijini Kigali, Rwanda.

Uongozi wa Yanga umempa mkataba wa miaka miwili Maximo kuchukua nafasi ya Mholanzi Hans Pluijm, ambaye amepata ajira mpya Al Shoallah ya Saudi Arabia pamoja na msaidizi wake, Boniface Mkwasa.