come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

GOMIS AJIUNGA NA SWANSEA

Bafetimbi Gomis

Klabu cha ligi ya Premier ya Uingereza, Swansea, wamesajili mshambuliaji maarufu ya Olympique Lyon ya Ufaransa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Gomis, 28, amejiunga na Swansea baada ya kandarasi yake na Lyon kukamilika.

“Swansea City wana furaha kutangaza kusainiwa kwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Bafetimbi Gomis kwa masharti ya kukamilisha hati ya uhamisho,” taarifa kwenye tovuti rasmi ya klabu hicho ilitangaza.

Swansea walijaribu kuleta straika huyo kabla ya mwanzo wa musimu jana lakini hawakufaulu na badala yake, walimsajili Wilfried Bony ambaye ameibuka kama pendo la mashabiki wa Liberty Stadium kwenye musimu ambao walimaliza nafasi ya 12.


Gomis, alisajiliwa na Lyon kwa dhamani ya milioni 13 sarafu za Euro mwaka wa 2009 na alizamisha magoli 22 musimu jana ingawa hakuorodheshwa na kocha wa Ufaransa kwenye kikosi chake cha Kombe la Dunia.