Chanzo chetu cha habari kimeshuhudia picha kadhaa za wawili hao wakiwa katika pozi fulani fulani za kimahaba, aidha mwandishi wa habari hizi alimwendea hewani msanii huyo ambapo alionekana kushangaa kidogo lakini baadaye alikiri.
'Nikweli nilikuwa naye lakini sina mahusiano yoyote ya kimapenzi, yule ni mmoja kati ya mashabiki wangu aliamua kupiga picha na mimi katika hali ile si unajua mapenzi ni mapenzi hata mama yako ni mpenzi pia, unajua watu wanachukulia mapenzi ni mahusiano ya kingono', alisema Mkali Fizo.
Hata hivyo picha nyingine zilizokutwa katika mtandao huo wa kijamii zilileta mshangao kwani zilionyesha wawili hao walikuwa kama kwenye chumba maalum wakifanya yao na wakati huo walionekana katika mapumziko fulani.
Jitihada za kumtafuta mrembo huo anayetokea mikoa ya kaskazini mwa Tanzania zilishindikana kufuatia simu yake ya mkononi kutokuwa hewani, mrembo huyo inasemekana alikwenda kushiriki mashindano hayo ya urembo lakini anatokea jijini Dar es Salaam