come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

EMMANUEL OKWI AKUBALI KUREJEA YANGA

MSHAMBULIAJI raia wa Uganda Emmanuel Okwi amekubali kurejea katika klabu yake ya Yanga na kuendelea kuichezea timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi inayotarajia kuanza Agosti 24 mwaka huu, kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu amesema kuwa Okwi ataendelea kuichezea Yanga.

Hivi karibuni kumekuwa na maelewano mabaya kati ya Okwi na Yanga kiasi kwamba kuleta hofu kwa mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani ambapo ilisemekana kuwa Okwi yuko tayari kuvunja mkataba wake na Yanga.


Hata hivyo mazungumzo kati ya Okwi na mwenyekiti wa klabu hiyo bilionea Yusuf Manji umeweza kusaidia kurejea kwake huku Yanga ikiahidi kumalizana naye, Okwi alikuwa akiidai Yanga jumla ya Mil 64 ambapo Manji amesema atammalizia.

Hivyo sasa hofu iliyotanda Jangwani kuwa straika huyo hatoweza kuwasili tena nchini imeondoka na muda wowote atajiunga na kikosi hicho kinachowania taji lake la 23 hapo Agosti huku pia ikijiandaa kuchezana Azam katika ngao ya Hisani.

Okwi alisaini mkataba wa mika miwili na nusu akitokea klabu ya Villa ya Uganda ambayo ilipewa kwa kibali maalum na shirikisho la kandanda la nchi hiyo FUFA baada ya kutokea malumbano kati ya Okwi na iliyokuwa klabu yake ya Etoile Du Sahel ya Tunisia ambayo ilimnunua toka klabu ya Simba ya Tanzania.