come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ARGENTINA YATAJA KIKOSI CHA MWISHO, DEMICHELIS NDANI...NAHODHA MESSI

BEKI wa kati, Martin Demichelis jana ameorodheshwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wa Argentina kitakachokwenda kwenye Kombe la Dunia, huku kiungo maarufu mkaa benchi, Ever Banega akitemwa.

Kocha Alejandro Sabella alimrejesha kikosini Demichelis katika kikosi chake cha awali mwezi uliopita baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England na Manchester City baada ya miaka miwili ya kuwa nje ya kikos cha Argentina.

Martin Demichelis amerejeshwa kikosini Argentina
Beki aliyempisha Demichelis ni mkongwe mwingine aliyecheza Fainali za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, Nicolas Otamendi, ambaye alikuwa anacheza kwa mkopo Atletico Mineiro ya Brazil ambaye pia alirejeshwa hivi karibuni na Sabella.


Winga wa Benfica, Enzo Perez pia ameopata nafasi ya kwenda Fainali za Brazil zinazoanza Juni 12, lakini Banega, ambaye alijiunga na Old Boys kutoka Valencia msimu huu, ametemwa kwa sababu ya kuwa mgonjwa na kushuka kiwango.

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, anatarajiwa kuiongoza timu yake kuwania Kombe la tatu la Dunia, wakiwa wamepangwa Kundi, F moja na Bosnia, Iran na Nigeria.

Kikosi kamili ni makipa; Sergio Romero (Sampdoria), Mariano Andujar (Catania) na Agustin Orion (Boca Juniors), mabeki; Pablo Zabaleta (Manchester City), Federico Fernandez (Napoli), Ezequiel Garay (Benfica), Marcos Rojo (Sporting Lisbon), Hugo Campagnaro (Inter Milan), Martin Demichelis (Manchester City) na Jose Basanta (Monterrey).

Viungo ni; Javier Mascherano (Barcelona), Fernando Gago (Boca Juniors), Lucas Biglia (Lazio), Ricardo Alvarez (Inter Milan), Augusto Fernandez (Celta Vigo), Angel Di Maria (Real Madrid), Maxi Rodriguez (Newell's Old Boys) na Enzo Perez (Benfica), wakati washambuliaji ni Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Sergio Aguero (Manchester City), Rodrigo Palacio (Inter Milan) na Ezequiel Lavezzi (Paris St Germain).