Kocha wa Brazil , Luiz Felipe
Scolari, amesema kuwa mshambulizi nyota wa Barcelona ya Uhispania na
Brazil Neymar alikumbwa na mshtuko na kuhofia kuwa alikuwa amepooza
miguu yake punde baada ya kugongwa uti wa mgongo na kiungo wa Colombia
Juan Zúñiga .
Scolari amewaambia wanahabari kuwa alikuwa
anasema kuwa miguu yake imekufa ganzi kabla ya kukimbizwa hospitalini
mjini Fortaleza ilikupigwa picha ya Xray.
Neymar alihofia kupooza
Daktari wa timu hiyo Rodrigo Lasmar
amedhibitisha kuwa Neymar amejeruhi uti wake wa mgongo na kuwa hatoweza
kucheza kwa kipindi cha majuma manne hadi 6 yajayo .
Kauli hiyo imemlazimi Scolari kupanga upya safu yake ya mashambulizi ilikufidia pengo aliyoiwacha Mshambulizi huyo machachari.
Neymar alikimbizwa hospitalini kwa helikopta
timu yake ilipokuwa ikiongoza 2-1 dhidi ya Colombia katika mechi ambayo
wenyeji hao walijikatia nafasi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Picha za mshambulizi huyo akilia ziliwatamausha mashabiki wake kote duniani .
Neymar alipojeruhiwa na Juan Zuniga
Mashabiki wa Brazil sasa wamesalia na hofu kubwa
kutokuwepo kwake huenda ikaifanya selecao kuwa wadhaifu mbele ya
Ujerumani timu hizo zitakapokutana sikua ya jumanne.
Scolari amesema kuwa ''Bila shaka tumempoteza
mchezaji ambaye anaweza kuleta tofauti kubwa mno katika mechi yeyote
ile hususan katika mechi hiyo ya jumanne dhidi ya Ujerumani''