Kesi ya mauaji inayomkabili
mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius imeanza kusikilizwa tena, huku picha
za video zinazomuonyesha mwanariadha huyo alivyomuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp zikiwa zimetolewa.
Mwanasheria Pistorius amevilaumu vyombo vya
habari vya Australian kwa kurusha picha hizo za video kwa madai kuwa
zilipatikana kinyume cha sheria.Mwandishi wa BBC nchini Afrika kusini anasema huenda ushahidi ulioonyeshwa kwenye picha hizo ukatumika katika mashitaka hayo ya Pistorius.
Picha hizo zimeonyeshwa jana katika runinga moja nchini Austarilia, msemaji wa Pistorius picha hizo zilichukuliwa kwaajili ya uchunguzi wa kisayansi japo kuwa ilikuwa katika mfumo ambao ni kinyume cha sheria.
"Kwa upande wa familia kurushwa kwa picha hizo ni kama kuingilia uhuru binafsi” anasema msemaji huyo. Hata hivyo picha hizo hazijawahi onyeshwa nchini Afrika Kusini ambako ndiko kesi hiyo imekuwa ikiendeshwa.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding aliyepo Africa Kusini anasema haifahamiki mara moja kwanini picha hizo hazikutumika kama kielezo katika kesi ya Pistorius.
Pistorius mwenyewe ameendelea kusisitiza kuwa alimuua mpenzi wake kwa bahati mbaya akidhani kuwa walikuwa wamevamiwa na majmbazi.
Mwanariadha huyo amekuwa katika mapenzi na Steenkamp kwa takribani miaka mitatu kabla ya mauajia hayo.