KOCHA
mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars Mholanzi Mart Nooij na Mbrazil
Marcio Maximo anayeinoa Yanga wameingia vitani kila mmoja akitaka kuona
taifa lake linaibuka mbabe wa soka duniani, Brazil na Uholanzi zipo
katika kombe la dunia linalofanyika nchini Brazil.
Huku timu hizo zote mbili zikifanikiwa kuingia nusu fainali, wakati
kesho Brazil ikicheza na Ujerumani, Uholanzi itakuwa na shughuri pevu
itakaposhuka uwanjani kukabiliana vikali na Argentina siku inayofuata
yaani Jumatano.
Maximo raia wa Brazil akiwahamasisha mashabiki wa Yanga kuishangilia
Brazil, Nooij naye amekuwa akiwahamasisha mashabiki wa Tanzania kuipenda
Uholanzi, makocha hao sasa wanaingia katika vita kubwa ambapo mshindi
ni yule ambaye taifa lake litafanya kweli na kuchukua kombe hilo
lililoachwa na watetezi Hispania ambao waliondolewa katika hatua za
mwanzo.
Haijulikani nani ataibuka mbabe katika michuano hiyo mikubwa kuliko yote
ulimwenguni lakini kila timu imepewa nafasi ya kushinda, Brazil kikosi
chake hakionyeshi soka safi kiasi kwamba kupewa nafasi finyu kuifunga
Ujerumani lakini haitabriki kutokana na kushinda mechi zake ngumu.
BNrazil iliifunga Colombia timu ambayo inacheza soka safi na la
kupendeza, Uholanzi nayo imeonyesha umahiri wa hali ya juu kiasi kwamba
mashabiki wa soka wanaipa nafasi kubwa kubeba ndoo huku Argentina
ikipewa nafasi finyu mbele ya Wadachi hao wanaouungwa mkono na kocha wa
Stars ambaye ni Mholanzi