Prodyuza anayechipukia ambaye ndiye aliyegonga wimbo bora wa My Number One wa super star Naseeb Abdul 'Diamond Plutinumz' Sheddy Clever ametangaza kuhamisha makazi yake Tabata na kuhamia jirani na Mlimani City.
Akizumgumza kupitia ukurasa wake wa Instragram, Sheddy amesema studio yake haipo tena Tabata na sasa amehamia jirani na Mlimani City hivyo amewataka wasanii na wadau wake kumfuata huko na wala wasiende tena Tabata kwani yeye hayupo tena.
Sheddy amewaasa wadau wa muziki pamoja na wasanii kutokwenda Tabata kwani ameamua kuhama jumla na vifaa vyake na ajaacha mtu yeyote aiendeleze studio yake, kwa sasa amehamia jirani na Mlimani City hivyo mtu yeyote atakayejtokeza na kudai Burn Record ipo Tabata huyo ni tapeli alisema Sheddy.
Baadhi ya wasanii wamekuwa wakienda katika studio yake hiyo ya zamani lakini kwa sasa yuko jirani na Mlimani alisisitiza, kumekuwepo na vitendo vinavyoashiria utapeli ambapo baadhi ya watu wamejitokeza na kudai wao ndio Burn Record na wanarekodi kwa gharama nafuu hivyo amewaasa mapema ili watu wasije kutapeliwa.