Timu hiyo iliyoondolewa na Costa Rica katika
mkondo wa pili ilimwandikia waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras barua
ikimtaka atumie fedha hizo kujenga uwanja mpya wa kandanda utakaotumika
kutambua na kukuza vizazi vipya vya kandanda.
Ugiriki iliambulia kichapo cha mabao 5-3 kupitia mikwaju ya penalti mikononi mwa Costa Rica.
Bwana Samaras aliahidi kutekeleza ombi la wachezaji wake alipozungumza kwa njia ya simu na maafisa wa shirikisho la soka la Ugiriki.
Bwana Samaras aliahidi kutekeleza ombi la wachezaji wake alipozungumza kwa njia ya simu na maafisa wa shirikisho la soka la Ugiriki.