come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MASHABIKI YANGA WAMKATAA OKWI

MASHABIKI na wapenzi wa klabu ya Yanga ambayo inajiandaa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati itakayofanyika nchini Rwanda mwezi huu wamependekeza jina la mshambuliaji wao Mganda Emmanuel Okwi akatwe katika orodha ya majina ya wachezaji watano wa kigeni.

Mashabiki hao wametoa mapendekezo yao kupitia gazeti la Kabumbu linalotolewa kila siku ya Ijumaa, gazeti hilo lenye itikadi za Yanga lilitoa nafasi kwa wasomaji wake ambao ni wapenzi wa Yanga kupiga kura ili nani akatwe katika ya Okwi na Kiiza.

Kura nyingi zilisema Okwi aachwe huku nyingine chache zikitaka Kiiza aachwe, mashabiki waliotaka Okwi aachwe wametoa  maoni yao kuwa Okwi ni msumbufu na ameshindwa kuonyesha mapenzi yake  kwa Yanga hivyo ni bora aachwe tu, na wale waliotaka Kiiza aachwe wamedai mchezaji huyo hakuwa na maelewano mazuri na wenzake na kusababisha Yanga kupoteza ubingwa wake.


Kura hizo ziliendeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu live ambapo mratibu wa zoezi hilo ni mwandishi wa habari wa gazeti hilo Fikiri Salum ambapo amedai wasomaji wengi wanmempigia simu huku wakitaka Okwi aachwe.

Yanga ina maproo wa kigeni sita ambao ni Emmanuel Okwi, Hamisi Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite, Genilson Santana Santos 'Jaja' na Andrey Coutinho, kusajiliwa kwa Jaja ndio kumepelekea kukatwa kwa jina la mchezaji mmoja wa kimataifa ambapo pendekezo liliwekwa na uongozi akatwe Kiiza au Okwi.