come
MAXIMO AIGAWA YANGA VIKOSI VIWILI, KIMOJA KAGAME KINGINE PEMBA
KOCHA wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo ameamua kuwatupia mzigo wa Kombe la Kagame wasaidizi wake, Leonardo Neiva na Shadrack Nsajigwa na kuwapa wachezaji 21 ambao anasema wana uwezo wa kurejea na kombe hilo Tanzania.
Lakini watani wa Yanga baada ya kusikia uamuzi wa Maximo wakaanza kukejeli kwamba amekimbia lawama ingawa yeye ameeleza wazi programu yake.
Wakati Neiva na Nsajigwa wakienda kupambana nchini Rwanda Maximo ataungana na kocha wa kikosi cha timu ya vijana ya klabu hiyo, Salvatory Edward kuweka kambi Pemba.
Yanga imepangwa kundi A katika michuano hiyo na itatupa karata yake ya kwanza Agosti 8 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.
Japo Maximo amefanya siri juu ya kikosi kitakachokwenda
kwenye kombe la Kagame, Tunafahamu kuwa wachezaji walioko na timu za taifa ni Oscar Joshua na Nadir Haroub Cannavaro
pekee watakaoungana na kikosi hicho.
Oscar anapewa nafasi kubwa ya kwenda kutokana na nafasi anayoicheza kuwa na mchezaji mmoja tu Amosi Abel kutoka timu ya vijana huku Cannavaro akienda kutokana na
kukosekana kwa beki mzoefu wa kati.
Mtandao huu unafahamu kuwa Katika wachezaji waliofanya mazoezi na Maximo tangu mwanzo watakaoenda Rwanda kwenye michuano hiyo ya Kagame kwa mujibu wa mazoezi ni makipa Juma Kaseja, Ally Mustapha ‘Barthez’ na Said Ally wa
timu ya vijana.
Mabeki watakaoongozana na kikosi hicho ni Juma Abdul, Said Juma, Rajab Zahir, Salum Telela, Issa Ngao, Amosi Abel, Oscar na Cannavaro. Viungo ni Mbuyu Twite na Omega Seme (kama viungo wakabaji) , Hassan Dilunga na Hamis Thabiti
kama viungo washambuliaji.
Wabrazil Andrey Coutinho na Genilson Santos ‘Jaja’, Saidi
Bahanuzi na Jerry Tegete ndio wakataoongoza safu ya ushambuliaji.
Jeshi la Yanga hilo: kocha Marcio Maximo anatarajia kuwa na vikosi viwili ambapo kingine kitashiriki kombe la Kagame na kingine kitaweka kambi Pemba
Wachezaji wengine watakaokwenda na kikosi hicho ni Nizar Khalifan na Hussein Javu ili kukamilisha idadi hiyo ya wachezaji 21. Maximo alisema, “Mimi sitakwenda na timu, watakwenda Nsajigwa (Shadrack) na Leonardo (Neiva) na
kikosi cha wachezaji kati ya 20 ama 21 pekee, kati ya hao mmoja au wawili pekee anayetoka kwenye majukumu ya kitaifa ndiyo watakaojiunga na timu.
“Mimi na Salvatory (Edward) tutasafiri na wachezaji wengine wanaotoka kwenye timu za Taifa pamoja na hawa wanaobaki kwenda Pemba (visiwani) kuweka kambi, tutafanya mazoezi
mpaka watakaporejea kutoka Kagame.”
“Watakaokwenda na timu Kagame wataandika ripoti na pia nitazitazama picha za video, baada ya hapo tutafanya tathmini na kupanga kikosi imara kwaajili ya mapambano,” alisema Maximo huku katika mazoezi ya jana wachezaji wa Yanga akiwemo Coutinho na Juma Abdul wakimchezesha Jaja kiutamu tofauti na siku za nyuma.