|
|
Straika matata wa Paris St Germain, Zlatan
Ibrahimovic, alifungia taifa lake Uswidi bao la 50 na kuweka rekodi mpya
ya mabao kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Estonia Alhamisi.
Sherehe zake za mahanjam kwa kufikia kilele hicho zilifanya alishwe kadi ya njano.
Ibrahimovic alisawazisha rekodi yake Sven Rydell ya mabao 49 alipotia kimyani dakika ya tatu na katika ya 24, akamiliki rekodi hiyo baada ya kupata lake la pili.
Alivuta shati yake kuonyesha ingine iliyoandikwa “Mabao 50” nyuma na “Ni nyinyi mliowezesha haya” lakini alipewa ya njano kwa madaha hayo.
Ilikuwa ni mechi yake ya 99 na nyota huyo, 32, atacheza yake ya 100 Jumatatu kwenye mechi ya kufuzu kombe la Ulaya dhidi ya Austria.