come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA, AZAM ZAIPIGA BAO SIMBA

AZAM FC ilimaliza ligi ya msimu uliopita ikiwa mabingwa huku Yanga SC ikikamata nafasi pili, Simba ilikamata nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City iliyokamata nafasi ya tatu, lakini safari hii tena Azam FC na Yanga SC zimeiliza tena Simba kivungine.

Azam fc na Yanga zimeipiku Simba na sasa zinafanya vizuri, unafikiri zimeipiga bao kwenye nini! shusha pumzi kwanza, vilabu vya Azam FC na Yanga SC zote za jijini Dar es salaam zinafanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na kuipoteza kabisa klabu ya Simba.


Yanga inamiliki mtandao wake na imekuwa ikiwapasha habari muhimu mashabiki wake kupitia page yake ya facebook na website, wana-Yanga wanapata habari za klabu yao kirahisi tu tofauti na wale wa Simba ambao husikilizia habari kupitia vipindi vya michezo.

Uongozi wa Yanga umerahisisha mambo na sasa matokeo ya mechi zake au taarifa muhimu imekuwa ikiwapa kupitia mitandao ya kijamii, sasa hivi watu wqengi uangalia mitandao ya kijamii kupitia simu zao za mkononi hivyo Wanayanga wanapata taarifa za klabui yao mapema.

Azam FC nayo inaenda kisasa na iikiwapa taarifa zake mashabiki wake kupitia page zake za Website na facebook, lakini Simba imeachwa mbali kwani hawaendi kisasa na wameachwa nyuma na utandawazi