come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

UFARANSA YATAKA KUJIPIMA ZAIDI KWA MECHI ZA KIRAFIKI

Didier Deschamps 

Wenyeji wa Euro 2016 Ufaransa watachukulia mechi za kujipima nguvu kwa ajili ya dimba hilo la mataifa 24 kana kwamba ni za kufuzu, kocha Didier Deschamps alisema Jumamosi.

Baada ya kulaza Uhispania 1-0 jijini Paris Alhamisi, Ufaransa watakutana Serbia mjini Belgrade Jumapili, ikiwa mechi ya kwanza kati ya nane dhidi ya mechi zilizo katika Kundi I la kufuzu kwa dimba hilo, likiwa kundi pekee lenye timu tano badala ya sita.

"Lengo ni kutwanga kila timu katika kundi na kupata alama za juu zaidi na hilo lina maana kwamba tutacheza kana kwamba hatujapewa nafasi ya moja kwa moja ya kfuuzu kwa fainali hizo,” Deschamps aliambia kikao cha wanahabari.

“Ndio njia pekee ya kufikia kilele cha uchezaji kabla ya michuano hiyo ambayo matarajio yatakuwa makubwa.


“Tuna miaka miwili ya kujiandaa na tutakuwa na kazi nyingi kufikia kiwango kinachohitajika,” mkufunzi huyo wa miaka 45, aliyekuwa wakati mmoja nahodha wa Ufaransa, alisema kupitia mkalimani.

Ufaransa walipendeza sana dhidi ya Uhispania baada ya kufika nane bora Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, na Deschamps alisema timu ilijifunza mechi na anatarajiwa wawe wa kupigiwa upatu kushinda Euro 2016 wakiwa wenyeji.

"Siku 50 tulizokuwa pamoja kabla na wakati wa Kombe la Dunia tulijifunza mechi na mchezaji yeyote anayeongezwa kwenye kikosi anaweza tu kukiongezea ukali, lakini wachezaji wapya watakaoingia watahitajika kupigania nafasi zao,” akasema.