come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DIAMOND AFANYA KUFURU, AMNUNULIA GARI MZEE GURUMO

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz (Akiwa pichani na mzee Gurumo) amemnunulia gari mzee Gurumo kama zawadi na heshima yake kwake kwa mzee huyo mkongwe wa muziki hapa nchini.


Mwanadada mtangazaji wa kipindi cha bongo movies nchini kinachooneshwa na kituo cha clouds TV Zamaradi Mketema ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya tukio hilo la aina yake na kihistoria hapa nchini na kuamua kuandika yafuatayo kwa Msanii huyu anayefanya vizuri katika mziki wa kizazi kipya kwa sasa.

Kupitia mtandao, Zamaradi ameandika…

“Mtu anapofanya kitu kizuri hatuna budi kumpongeza... ameshafanya mazuri mengi, makubwa mengi na anaendelea kufanya mengi ya kuigwa..

amefanikiwa kuonesha taswira nyingine kabisa ya muziki wa bongo fleva.. ameweza kuprove kwamba kupitia MUZIKI tu unaweza kuishi na kufanya big things.. kiufupi amekuwa role model wa wasanii wengi.

Wanaoanza muziki in EVERYTHING!!! As i said umefanya makubwa mengi lakini hili la kumnunulia Gari mzee Gurumo ambae alikuwa kwenye muziki kwa miaka 53 na hakufaidika chochote na muziki wake linaweza likaonekana la kawaida lakini kwa yeye KUWAZA na KUFANYA kitu cha aina hiyo anastahili pongezi kubwa sana kwakweli..ni moja kati ya makubwa na ya maana uliyoyafanya mwaka huu