Na Prince Hoza
MDAU maarufu wa vipindi ya redio hapa jijini Beatrice Shadrack ama
eatrie wa Kariakoo ukipenda Sister dread wa ukweli Mama Balotelli wa Tz
(Pichani) amenusurika kufa asubuhi ya leo baada ya kupata ajali mbaya ya
pikipiki.
Akizungumza na mtandao huu Peter Tosh ambaye naye ni mdau wa media
amesema kuwa Mama Balotelli alipata ajali ya pikipiki katika maeneo ya
Buguruni.
Inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa pikipiki ndio umechangia kutokea kwa
ajali hiyo, Ingawa mpaka sasa mdau huyo maarufu katika vituo vya redio
anaendelea vizuri baada ya kupata huduma ya kwanza ila ameumia mguu wake
wa kulia