Na Charles Chinguile
CHIPUKIZI kwenye muziki wa kizazi kipya Edson Tumwandi a k a Dogo Tano amefanikiwa kutengeneza singo yake ya 'Tujitume' akiwa amemshirikisha mkali Ney wa Mitego, Akizungumza na KABUMBU SPOTI, Tano amesema kuwa wimbo wake huo umebeba ujumbe mkubwa kwa jamii.
Wimbo huo ulionogeshwa na msanii maarufu wa Hip hop Ney wa Mitego unaweza kufanya vizuri katika vituo vua redio, Msanii huyo anatarajia kuisambaza nyimbo yake hiyo kwenye vituo vya redio hivi karibuni huku mipango ya kutengeneza video iko mbioni.
Wimbo huo umetengenezwa kwenye studio za Burn Record zilizopo Tabata jijini chini ya prodyuza chipukizi Sheddy Clever