come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SAMIR WA KINYULINYULI KUKAMUA MOROGORO

Na Elias John

STAA anayechipukia kwenye muziki wa kizazi kipya Fadhil Kimbendela ama Mkali Fizo anatarajia kufanya shoo katika mji wa Morogoro ifikapo Juni 24, Akizungumza na MAMBO UWANJANI, Mkali Fizo amesema kuwa ameanza kupata mialiko mbalimbali baada ya wimbo wake wa Maisha Mtihani kukubalika.


Ameongeza kuwa katika shoo yake hiyo anatarajia kuambatana na msanii anayekuja juu kwa sasa Samir ambaye anatamba na wimbo wake wa Kinyulinyuli, Katika shoo hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Morogoro.
                                                                                                Samiri
Mkali Fizo amedai atafanya shoo ya uhakika na kukonga nyoyo mashabiki wake wanaomkubali, 'Nyimbo yangu ya Maisha Mtihani imeonyesha kukubalika katika vituo kadhaa vya redio hasa huko Morogoro ambapo mashabiki walitaka niende kufanya shoo', alisema Mkali Fizo.

Pia Mkali Fizo na Samir watatumia nafasi hiyo kutambulisha nyimbo zao mpya ambazo zinatarajia kutoka hivi karibuni, Mkali Fizo amedai wimbo wake mpya alioshirikiana na Rich Mavoko uitwao Tatizo Moyo atautambulisha kwa mashabiki wake siku hiyo.

Wakati Samir anayetamba na singo yake ya Kinyulinyuli naye ataitambulisha kwa mashabiki wake singo hiyo huku akishuka na nyimbo nyingine ambazo ziko mbioni kutoka, Kwa sasa nyota hao wanafanya mazoezi makali ili kudondosha shoo kali na ya kuvutia


Mkali Fizo kulia akiwa na mmiliki wa tovuti ya MAMBO UWANJANI, Prince Hoza