KLABU za Real Madrid na Barcelona zinamtaka beki wa kati wa Chelsea, David Luiz.
Mbrazil huyo anaweza kuwa lulu mbele ya kocha mpya anayekuja, Jose Mourinho ambaye amevutiwa na uwezo wake katika nafasi ya ulinzi.
Luiz aliigharimu Chelsea Pauni Milioni 21 nna watataka faida ikibidi kuuuza bidhaa hiyo waliyoinunua mwaka 2011.

Mpiganaji: Beki wa Chelsea, David Luiz alisajiliwa kwa Pauni Milioni 21 kutoka Benfica
Mourinho
anataka beki mpya wa kati, kiungo mkabaji na angalau mshambuliaji mmoja
katika kurejea kwake Stamford Bridge. Luiz amekuwa akitumika kama
kiungo mkabaji chini ya Rafa Benitez na imemsaidia kupunguza makosa yake
wakati anacheza kama beki.
Chelsea
imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji anayetakiwa na Liverpool,
Krygiakos Papadopoulos wa Schalke, lakini inamchukulia kinda huyo wa
miaka 21 kama ghali sana. Mourinho ni shabiki mkubwa wa Raphael Varane
wa Real Madrid pia, lakini suala hilo litaingiliwa na siasa zake za
kuondoka Bernabeu.
Tayari, wanaonekana kuimarisha safu yao ya ulinzi wakiwa na Branislav Ivanovic ambaye pia anawezwa kuhamishiwa beki ya kulia.

Kipaji: Raphael Varane wa Real Madrid (akipiga juu) anakubalika mno mbele ya Mourinho

Kazi ya kwanza ya Jose Mourinho Chelsea itakuwa kuimarisha safu ya ulinzi
Madrid
itakijenga upya kikosi cha Mourinho kupitia kwa Carlo Ancelotti.
Watakuwa tayari kumuuza beki Pepe kuliko Varane na Manchester City
wamepewa ofa ya kumsajili beki huyo Mreno kwa Pauni Milioni 20.
Kwa
upande wao, Barcelona wanapambana kuwania saini ya beki wa kati ambaye
hatazidi Pauni Milioni 25. Luiz yumo kwenye orodha yao muda mrefu,
lakini si kipaumbele cha mwanzoni.

Mourinho atatakiwa kuamua mustakabali wa John Terry na Frank Lampard msimu ujao
Walimtaka
Thiago Silva kutoka Paris St Germain, lakini ni ghali mno wakati
Manchester City hawako tayari kumuuza Vincent Kompany. Barca inamtaka
beki kinda wa Roma, Marquinhos lakini anaweza kuwa tayari kubaki kwa
msimu mwingine Italia.
Thomas
Vermaelen wa Arsenal anaweza kurejesha makali yake, lakini kumaliza
kwake msimu vibaya kunamfanya Luiz awe midomoni mwa watu zaidi yake.


Vincent Kompany kushoto na Thiago Silva kulia

Thomas Vermaelen amekuwa akimulikwa na Chelsea