LAZIMA
tuamini kwamba aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa amejiunga na
Yanga na ataichezea timu hiyo michuano yoyote itakayoshiriki kuanzia sasa.
Ngassa
amejiunga na Yanga huku kukiwa na vitimbi kadhaa vilivyotokea tangu anaondoka
katika timu hiyo miaka michache iliyopita, wakati huo Yanga ilikuwa chini ya
Mwenyekiti, Iman Madega.
Winga
huyo aliondoka Yanga na kujiunga na Azam FC katika usajili ambao haukutarajiwa
na wengi kutokana na mapenzi ya Ngassa kwa Yanga, bila shaka fedha iliongea. Azam
ililipa zaidi ya Sh. 90 milioni ili kumnasa mchezaji huyo.
Mwaka
jana katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, akiwa anaichezea
Azam, Ngassa baada ya kuifungia bao muhimu timu hiyo katika nusu fainali, alikwenda
kwenye kibendera cha kona na kukibusu. Kibendera hicho kina rangi ya kijani na
njano, rangi hizo zinatumiwa na Yanga.
Hiyo
ilionekana kama ishara ya kuitukuza Yanga na kuidharau Azam timu inamlipa
mshahara na posho nyingine, kwa kifupi ni mwajiri wake. Azam haikupendezwa na
hali hiyo, kabla ya kuanza kwa msimu huu ikatangaza kumtoa kwa mkopo kwa Simba.
Wakati
Azam inatangaza kumtoa kwa mkopo au kumuuza Ngassa, nilijua fika kwamba Yanga
inaweza kutia mkono wake hivyo ikatazama mazingira ya kumkwamisha kurejea
katika klabu yake na kuhakikisha anakwenda Simba.
Alipokuwa
Simba, Ngassa alipata ‘deal’ la kujiunga na klabu ya El Merreikh ya Sudan, viongozi
wa Simba walizungumza na El Merreikh bila ya kupata ridhaa ya Ngassa. Mwisho
wake mchezaji alikataa kujiungana timu hiyo ya Sudan.
Azam
ambayo nayo ingefaidika kama Ngassa angejiunga na El Merreikh, ni wazi
haikupendezwa na hali hiyo ya Ngassa kukataa kuiunga na klabu hiyo. Mkakati
ukapangwa.
Lakini
wakati haya yakitokea siku za nyuma hebu tutazame namna Ngassa alivyosajiliwa
na Yanga huku kukiwa na mambo kadhaa ya kushangaza;
NGASSA
HAJAPIMWA AFYA
Kama ilivyo kawaida ya timu nyingi za Tanzania, safari hii Ngassa amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili bila ya kupimwa afya…!
Jambo
hili la wachezaji kusajiliwa bila kupimwa afya sasa linaonekana la kawaida
ambalo klabu zimerithi utaratibu huo toka zamani, Dunia imebadilika lakini
viongozi wengi wa soka hapa nchini hawatazami hili.
Kwa
mfano Ngassa anaweza kuwa na matatizo ya afya katika viungo vyake vya mwili
ambavyo baadaye anaweza kuigharimu klabu kumgharamia matibabu kwa mfano matatizo
ya goti.
Matibabu
hayo yanaweza kuigharimu klabu kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingeweza
kufidiwa wakati wa usajili wake.
Kama
inavyodaiwa kwamba, Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba,
baada ya deal la kumpeleka El Merreikh kushindikana, Simba na Azam ziliamua
kupeleka mkataba huo wa Simba kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili
kuusajili ili Ngassa asiwe na uamuzi mwingine atakapoamua timu ya kujiunga nayo
mkataba wake utakapoisha Azam.
Lengo
la Azam na Simba lilikuwa ni kuona Ngassa hajiungi na Yanga na anaichezea Simba
msimu ujao pia, HATA KAMA BILA RIDHAA YAKE.
Kwa
kuwa Ngassa anafahamu anachofanya na anaheshimu maamuzi yake, aliamua kusaini
kuichezea Yanga ili acheze soka kwa amani zaidi.
Usajili
wa Ngassa kwa Simba (kama kweli alisaini) ulikuwa wa kama ‘kishika uchumba’ ili
awe na uhakika na ahadi ya kusajiliwa na klabu hiyo, hivyo baadaye angeweza
kuwa na maamuzi mengine kama alivyofanya sasa.
NGASSA
NI HALALI YANGA
Kama
kweli TFF itafuata hatua kwa hatua katika kile kinachoitwa mkataba wake na
Simba, Ngassa ataichezea Yanga msimu ujao, kwani kuna vitu vingi vilifanyika
katika mkataba huo bila ridhaa ya mchezaji.
Jambo
hili linaweza kuwa kama la usajili wa Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.