Mabingwa: Bayern Munich wakisherehekea taji lao la Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Borussia Dortmund
WINGA Arjen Robben ameuzika mzimu wa
kukosa penalti msimu uliopita katika fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi
ya Chelsea, baada ya usiku huu kuifungia bao la ushindi Bayern Munich
katika fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Wembley, London, England
ikishinda 2-1 na kutwaa Kombe hilo.