KLABU ya Manchester City imeitandika mabao 5-3 Chelsea katika mchezo wao wa pili na wa mwisho kwenye ziara yao ya Marekani jana kwenye Uwanja wa St Louis baada ya Alhamisi pia kushinda 4-3 kwenye Uwanaj huo huo dhidi ya The Blues.
Mabao ya City
yalifungwa Barry dakika ya tatu, Nasri dakika ya 29 na 73, Milner
dakika ya 54 na Dzeko dakika ya 84, wakati wa Chelsea yalifungwa na Ramires dakika ya 48 na 68 na Mata dakika ya 82.
Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart/Wright
dk45,, Zabaleta/Maicon dk45, Kompany/Lescott dk45, Boyata/Garcia dk55,
Kolarov, Yaya Toure/Rodwell dk45, Barry, Nasri, Tevez/Razak dk45,
Silva/Milner dk45 na Aguero/Dzeko dk45.
Chelsea: Hilario/Cech
dk45, Azpilicueta, Christensen, Luiz/Mata dk61, Ake, Mikel,
Loftus-Cheek/Ferreira dk42, Ramires, Oscar/Benayoun dk65, Ba na Torres.