![]() |
|
|
|
Baada ya kuwa mmoja wa waliolimbikiziwa lawama kufuatia
matokeo mabaya Kombe la Dunia 2010, golikipa Julio Cesar amejipata
akisifiwa tena Brazil baada ya kuchangia sana katika ufanisi wa Selecao
hadi kufika fainali Kombe la Confederations.
Mchezaji huyo mkongwe zaidi kwenye kikosi ambacho hakina uzoefu sana huku kocha Luiz Felipe Scolari akiendelea kuunda timu ya kuinua Kombe la Dunia nyumbani, akiwa na umri wa miaka 33 alifika kwenye dimba hilo baada ya kuaibika kufuatia kushushwa ngazi kwa timu yake ya Queen's Park Rangers kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.
Nyota ya jaha haikumwangazia kipa huyo mkongwe kutoka Duque de Caxias alivyokuwa ametarajia, alipokuwa akijiandaa kwa dimba la mwisho wa msimu la kujipasha moto kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Lakini amekuwa shujaa baada ya kuokoa penalti wakati wa ushindi wa nusufainali wa Jumatano dhidi ya Uruguay na kusaidia timu yake iliyokuwa ikitatizika kushinda kwenye uwanja wa Mineirao mjini Belo Horizonte.
Mpira aliozuia kutoka kwa Diego Forlan ulifanya asifiwe hata baada ya kipigo hicho kibaya kwa kocha wa Uruguay Oscar Tabarez, aliyekubali kushindwa na kusema Cesar “kwa mara nyingine alionyesha ni kipa stadi.”
Uchezaji wa Julio Cesar umekumbwa na misukosuko tangu alinde lango mara ya kwanza katika timu ya Flamengo misimu 16 iliyopita.
Bingwa huyo wa dunia wa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 mwaka 1997 alichezea Brazil mara ya kwanza 2004, na kuishindia Copa Amerika – alipookoa mkwaju wa penalti dhidi ya Argentina.
Ingawa kwa kiasi kikubwa alionekana kuwa wa pili baada ya Dida, alivutia Inter Milan, ambao mara ya kwanza walimtuma Chievo kwa mkopo.
Lakini alirejea miezi michache baadaye na kufanya mapinduzi dhidi ya Francesco Toldo na kuwa kipa nambari wani San Siro na baada ya kusaidia nchi yake kushinda Kombe la Confederations 2009, uchezaji wake ulifika kilele kufuatia ushindi wa Iner wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya 2010.
Licha ya hayo, wiki chache baadaye alilaumiwa kwa kuruhusu bao la Wesley Sneijder katika kipigo cha robofainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi na baada ya Mano Menezes kuwa kocha kuchukua pahala pa Dunga.
Adhabu yake ilifikia kikomo mapema mwaka huu baada ya Scolari kuingia kuchukua pahala pa Menezes na amejijengea sifa kama Nambari 1 kwenye wavu.
Kuhusu kuokoa kwake penalti dhidi ya Uruguay, Julio Cesar, ambaye anakaribia sana kufikisha mechi 100, alisema alifanya tu kazi yake na kwamba alijua Forlan angepiga penalti yake upande wa kushoto.
"Nilicheza naye Inter Milan – lakini pia nilifanya kazi nzuri," aliambia wanahabari.
"Kwa bahati, Julio Cesar aliokoa penalti hiyo vyema sana,” aliongeza mchezaji mwenzake wanayecheza pamoja London, difenda wa Chelsea David Luiz, ambaye madhambi aliyomfanyia Diego Lugano yalisababisha penalti hiyo.
Julio Cesar amefanikiwa kuondoa masaibu yake siku za hivi majuzi akiwa QPR na akiwa Brazil na sasa ana mechi moja tu kati yake na kushindia taifa lake taji la tatu la kimataifa.
Lakini atakuwa akitumaini kuwa ufanisi wake halisi utakuja miezi 12 kutoka sasa Brazil ikilenga taji inalosaka kuliko yote: Kombe la Dunia la sita.