come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PATA MAKALA YA KELVIN PATRICK YONDAN

Beki bora Tanzania, Amwaga chozi kumlilia Mangwea

MASHABIKI wa Simba SC bado wanakosa raha kutokana na timu yao kuwa katika mapungufu makubwa katika idara yao ya ulinzi, Simba imeshindwa kupata beki imara anayeweza kulinda heshima ya klabu hiyo.


Na ukifanya tathimini za haraka haraka hakuna uwezekano wa Simba kupata beki imara kama ilivyowahi kuwapata mabeki imara na visiki kama Deo Njohole, Seleman Pembe, George Masatu, Willy Martin, Boniface Pawassa, Victor Costa na baadaye Kelvin Yondan.

Yondan anatajwa kama beki bora wa kihistoria kuwahi kuichezea Simba na Tanzania kwa ujumla, Na mbadala wake inahitajika bidii ya miaka zaidi ya kumi au zaidi ili kuweza kupata mtu sahihi katika idara ya ulinzi.

Wataalamu wa masuala ya soka wanasema kumpata beki kama Yondan inahitaji muda, Simba ilishindwa kusimama imara msimu uliopita licha ya kuhangaika huku na kule kutafuta mbadala wa Yondan.

Ilipoona imeshindwa kumpata beki kama Yondan iliamua kwenda TFF kulalamikia kitendo cha beki huyo kujiunga na Yanga, Simba walidai Yondan ni mchezaji wao kihalali.

Lakini baadaye wakaumbuka mbele ya Alex Mgongolwa ambaye alithibitisha kuwa mchezaji huyo ni mali ya Yanga kwani mkataba wake na Simba ulishamalizika.

Simba walianza mchakato wa kutafuta mabeki ambapo ilisafiri hadi Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kufanikiwa kumchukua beki kisiki Lino Musombo, Musombo alipotua katika ardhi ya Tanzania alianza kupambwa kwenye kurasa za magazeti ya michezo yenye sifa za kupamba wachezaji hata kama haijawahi kuwaona huko walipo.

Musombo alisifiwa sana na mashabiki wa Simba ambao mimi nakula nao na kushinda nao kijiweni walijikuta wanapumua hasa kwa kumpata mbadala wa Yondan.

Lakini alipoanza kuingia uwanjani kuitumikia klabu ya Simba, Musombo alikuja kuonekana 'garasa' baada ya kucheza chini ya kiwango, Simba waliamua kumtimua na kuendelea na mchakato wa kutafuta beki mwingine ili kuja kuziba pengo la Kelvin Yondan.

Viongozi wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba waliojaa porojo nyingi kama ilivyo kwa wachekeshaji maarufu nchini Joti na Mpoki, Walielekea nchini Kenya kumfuata beki Pasckal Ochieng.

Ochieng aliwasiri nchini kuanza kibarua cha kuitumikia klabu ya Simba na baadaye ikaongezewa nguvu na Komalbili Keita kutoka nchini Mali, Simba wakawa na furaha ya kupata mabeki na kuunda ukuta imara kama ule iliokuwa nao huko nyuma.

Kelvin Yondan alicheza vema na Juma Nyosso na kuifanya Simba kuwa na beki imara katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, Lakini baadaye Simba ikajikuta inapoteza mwelekeo na kufikia ya kuwasitishia miakataba yao nyota hao wa kimataifa.

Na sasa imeamua kumleta beki mwingine kutoka nchini Uganda ili mradi kuziba pengo la Yondan, Lakini ukweli utabakia kuwa Yondan ni beki bora hapa nchini na Afrika mashariki na kati kwa ujumla.

TEGEMEO LA KIM POULSEN

Safu ya ulinzi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayonolewa na Mdenmark Kim Poulsen mtu wa kwanza anayeaminika ni Kelvin Yondan, Poulsen humwambii kitu kwa beki huyo.

Amekua akimpa majukumu makubwa ya kuiongoza safu ya ulinzi na kutokana na uelewa wake, Yondan ameweza kuyaelewa maagizo ya mwalimu wake, Alianza kupewa jukumu la kusimama katika idaya ya ulinzi tangia alipokuwepo Mbrazil Marcio Maximo na aliweza kushirikiana vema na Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Na sasa anashirikiana na Aggrey Morris, Na wameweza kutengeneza ukuta imara ambao umeshindwa kupitika, Stars imecheza na timu ngumu na kubwa barani Afrika zenye wachezaji wanaocheza soka la kulipwa Ughaibuni lakini zote hizo zenye washambuliaji wenye uchu wa kufunga mabao wameshindwa kuupita ukuta unaoongozwa na Kelvin Yondan.

PAMBANO LAO NA MOROCCO JUN 8

Kwa sasa Kelvin Yondan yuko nchini Morocco pamoja na kikosi cha timu ya taifa kwanza amewatoa wasiwasi mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa wakiulizia habari za wachezaji wao kama wamesaini au laah.. Yondan amesema yeye ni mchezaji wa Yanga na ataendelea tena kuitumikia klabu yake msimu ujao.

Akielezea mpambano wao dhidi ya Morocco, Amedai Stars imejiandaa vema na mchezo huo na Watanzania watarajie ushindi, 'Ingawa tunacheza ugenini lakini ushindi utapatikana kwani Morocco ni timu ya kawaida sana na wala haitutishi', alisema.

Aliongeza kuwa wanaiheshimu sana Morocco kutokana na heshima yake kisoka barani Afrika lakini wataionyesha kazi kwani Tanzania ni kizazi kipya cha soka Afrika.

KIFO CHA MSANII MANGWEA

Kwanza alikipokea kwa msikitiko makubwa kifo cha msanii huyo na kuinyesha hisia zake kuwa ameguswa sana na kifo chake, Mangwea alikuwa msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na wachezaji wanapopata nafasi ya kupumzika hupendelea muziki.

'Mimi ni mmoja kati ya mashabiki wake na nilikuwa nikifuatilia sana muziki wake, Hata nyakati za mapumziko huwa (likizo)  nasikiliza ngoma zake, Mungu amlaze mahara pema peponi Amina, (huku akimwaga chozi).

Yondan amewataka Watanzania kuwaombea kwa mungu ili waweze kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Morocco utakaopigwa Jumamosi ya tarehe 8