come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BREKING NEWS: WAMBURA AREJESHWA SIMBA

KAMATI ya TFF imetangaza kumrejesha aliyekuwa mgombea wa urais katika klabu ya Simba kabla ajaenguliwa Michael Wambura kuendelea tena katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.


Taarifa zilizotufikia hivi ounde zinasema kuwa Wambura amerejeshwa katika kinyang'anyiro hicho na atakuwa mgombea wa nafasi hiyo ya urais, sasa wagombea wa urais katika klabu ya Simba wamefikia watatu baada ya Wambura kurejeshwa.

Wagombea waliopo ni pamoja na Evans Aveva, Andrew Tupa na Michael Wambura, Wambura alienguliwa na kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba inayoongozwa na wakili Damas Daniel Ndumbaro ambapo baadaye Wambura alikata rufaa TFF kupinga kuenguliwa kwake.

Inasemekana Wambura hakuwa mwanachama halali kufuatia kusimamishwa kwake uanachama mwaka 2010 baada ya kuishitaki klabu ya Simba mahakamani wakati sheria za soka kimataifa zinapinga mwanachama yeyote kupeleka masuala ya soka katikia mahakama za dola