come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

FALCAO AKATA MZIZI WA FITINA, HATI YAKE YA KUZALIWA YAANIKWA HADHARANI

Radamel Falcao

Mjadala kuhusu umri halali wa nyota wa Colombia, Radamel Falcao ulisitishwa Alhamisi baada ya vyombo vya habari nchini humo kuchapisha nakala ya hati yake ya kuzaliwa.

Kizungumkuti hicho kilizinduliwa na aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule alimosomea ambaye aliambia kituo cha televisheni, Noticas Uno, kuwa Falcao alizaliwa mwaka wa 1984 badala ya ule wa 1986.
Tuhuma hii iliachilia umri wake kama 29 wala si 27, kumaanisha kuwa Monaco walitoa milioni 60 za sarafu ya Euro kwa mchezaji ambaye unri wake wa kustaafu ni miaka mbili zaidi ya ilivyoaminiwa.
Gazeti la El Tiempo lilichapisha nakala ya hati yake rasmi ya kuzaliwa kutoka manispaa ya Santa Marta alipozaliwa mnamo Februari 10, 1986 kudhibitisha kuwa Falcao ni miaka 27.
Jumanne iliyopita, Falcao alikanusha katika mtandao wa Twitter madai hayo akieleza kushangazwa kwake na ripoti hizo alizozipuuzilia kama tuhuma za ujinga.