come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PAPPISS CISSE AMALIZA UTATA WA JEZI

Papiss Cisse

Mshambuliaji wa Newcastle, Pappiss Cisse ameripotiwa kukubali kuvaa jezi ya kilabu hicho cha Ligi Kuu Uingereza ambayo ina alama ya kampuni ya wekezaji dau ya Wonga licha ya kukataa hapo mbeleni kuhusiana na dini yake.

Cisse alijiondoa kutoka ziara ya Newcastle Ureno baada ya kuambia timu hiyo hayuko tayari kukuza kampuni hiyo ya amana ambao wamechukua mahala pa Virgin Atlantic- ambao pia huhusika na huduma za amana-kama wafadhili wa msimu ujao kwasababu ya kutafarukiana na imani yake kama Mwislamu.
Walakini baada ya mazungumuzo ya wiki kadhaa, nyota huyo wa Senegal ameshawishiwa kurejea bomani kulingana na ripoti zilizochipuka Alhamisi.
Newcastle bado hawajadhibitisha maendeleo haya lakini duru zilizo karibu na mchezaji huyo zimesema anatarajiwa kurejea mazoezini na wenzake Ijumaa.
Kurudi kwa Cisse kutakuwa kigezo muhimu kwa meneja wa Newcastle, Alan Pardiew, ambaye ameshindwa kuwasajili straika wapya licha ya kusisitiza hio ndio juhudi angepatia kipao mbele baada ya msimu jana kukamilika.
Cisse aliwasili St James’ Park Januari mwaka jana katika shughuli iliyogharimu pauni milioni tisa kutoka kilabu cha Ujerumani, Freiburg na aliweza kuwa nyota mara moja baada ya kuzaba mabao 13 katika mechi 14.
Alipata ugumu kurudia onyesho hilo msimu jana lakini anabaki kama tegemeo la timu yake.