come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MOURINHO AWA MPOLE KWA ROONEY

Jose Mourinho

Meneja wa kilabu cha Ligi ya Uingereza, Chelsea, Jose Mourinho amesema ametulia kuhusiana na azima yake kuu ya kumsajili Wayne Rooney baada ya straika chipukizi, Romelu Lukaku kuzidi kungara na mabao mengine mawili huko Jakarta.

Mourinho alisisitiza hajawasilisha ombi lingine la kumsaini Rooney baada ya kilabu chake Manchester United kukataa lile la kwanza lakini aliongeza Chelsea wataendeleza msimamo wao wa kutolenga wachezaji wengine.
“La,” Murinho alinena baada ya Chelsea kuzaba Indonesia All Stars 8-1 alipoulizwa kama kuna maendeleo yeyote katika juhudi za kuwasajili wachezaji wapya.
“Kwa sasa, tuna yale mnayojua. Ombi hilo limo hadharani na ni rasmi na baada ya hapo, hakuna lingine isipokuwa utulivu. Tuko watulivu kwani tumerithika na wale tuko nao sasa.”
Meneja huyo wa Ureno ameanika matarajio mengi kwa kumsajili Rooney huku Chelsea wakitazamia kuto ongezea wengine baada ya kusaini Andre Schurrle, 22, wa Ujerumani, kiungo wa kati wa Uholanzi, Marco can Ginkel, 20 na goli kipa raia wa Australia, Mark Schwarzer, 40.
Mounrinho amefaidika na kurejea kwao viungo wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne na Lukaku waliorejea kutoka mikopo msimu jana. Lukaku amezaba mabao manne katika ziara yao ya bara Asia ambapo wamecheza mechi tatu.
Mourinho alizidi kuongeza kuwa straika ghali wa Uhispania, Fernando Torres, aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 50 atapata ushindani mkubwa kuanza mechi kutoka Lukaku hata bila ya kuongezwa Rooney katika kikosi.
“Fernando anafaa kufurahia ushindani katika timu yetu na hilo ni jambo nzuri kwa kila mechezaji katika kila kitengo.
“Fernando atanogeshwa kwasababu kwa muda, alikuwa straika mdogo katika Chelsea lakini baada ya hapo, Demba Ba aliwasili Januari na sasa tuna watatu.”
Alidokeza kuwa kiungo matata wa kati kutoka Unigereza, Frank Lampard, atarejea mazoezini wiki ijayo baada ya kuuguza jeraha la guu huku Chelsea wakisafiri Marekani kwa mechi zingine nne za kutangulia msimu ujao. Kilabu hicho kilitwaa taji la Ligi ya Uingereza katika msimu wa kwanza baada ya Mourinho kujiunga nao mara ya kwanza na hivi sasa wanaonekana kama tisho kuu la mabingwa wa sasa, Manchester United na waliowatangulia mwaka jana, Manchester City ambao pia wameajili meneja wapya hivi majuzi.