![]() |
“Kwenye kikosi cha sasa cha Yanga kuna wachezaji wangapi wa Simba, wengi tu, yule Barthez (Ally Mustafa), Yondan (Kevin), Chuji (Athumani Iddi) na bado walitaka kuwasajili Amri Kiemba na Shomary Kapombe,”.
“Usisahau Mbuyu Twite ni mchezaji ambaye tulikwishHamsajili sisi, wao wakacheza faulo na kumchukua juu kwa juu. Sasa namna hii hatuwezi kukuza soka na ushindani hata wa utani wetu wa jadi,”.
“Lazima Yanga iwe na wachezaji wake na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wake, na sisi tuwe na wachezaji wetu na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wetu,”.
“Ona kama sasa, sisi tumesajili mfungaji bora wa Kombe la Kagame, wao wameleta mfungaji bora wa Nigeria, sasa hawa watu wawili washindane kuzipatia matokeo mazuri timu hizi,”.
“Namna hii ndiyo mpira wa Tanzania utakuwa na si kusikia Simba kamfuata mchezaji na wewe unapeleka fedha zaidi kwa huyo huyo mchezaji, yale yalikuywa mambo ya kitoto na ya kishamba kabisa, ila sasa nawapongeza watani, wanaanza kukua,”alisema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Siku chache baada ya Simba SC kumpa Mkataba wa miaka miwili mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Amisi Tambwe wa Vital’O ya Burundi, Yanga SC nayo imeleta mpachika mabao hatari wa Nigeria, Chukwudi kutoka Heartland, aliyetua nchini usiku wa jana.
