KIONGOZI wa kundi la TMK Wanaume Halisi, Juma Natute 'Kibra' (Pichani) ameibuka na wimbo mpya unaohusiana na milipuko ya mabomu yanayoendelea kutokea hapa nchini mara kwa mara na kuashiria uvunjifu wa amani uliokuwepo tangia enzi.
Wimbo huo aliowashirikisha wasanii mbalimbali wa kundi lake la Wanaume Halisi, Nature pia amemshirikisha nguli wa Wagosi wa Kaya Mkoloni ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kuichana serikali kwa kushindwa kuwazuia waharifu.
Nature ametumia kufikisha ujumbe kutokana na mauaji yanayoendelea hapa nchini yatokayo na ulipuaji wa mabomu unaofanywa na watu wasiojulikana, Licha ya kutofahamika watu hao Serikali imekuwa ikiwakamata wanaohusika lakini hakuna kinachoendelea zaidi ya hapo.
Tayari wimbo huo umeanza kukubalika mbele ya jamii na kujipatia mashabiki wengi.
Habari na Fikiri Salum