KLABU ya Manchester City ipo mbioni kumnunua kwa Pauni Milioni 28, nyota wa Fiorentina, Stevan Jovetic.
Pamoja na hayo, City imepata pigo katika
mpango wake wa kumsajili Alvaro Negredo, baada ya rais wa Sevilla, Jose
Maria del Nido kuonya kwamba hakuna hata asilimia moja ya uwezekano wa
dili hilo kufanikiwa.
Kocha mpya, Manuel Pellegrini anataka
kusajili washambuliaji wawili kuziba pengo la wachezaji walioondoka hivi
karibuni, Carlos Tevez na Mario Balotelli.

Ndani na nje: Alvaro Negredo anakwenda Man City, lakini Stevan Jovetic yuko njia panda

Dukani: Kocha mpya wa City, Manuel Pellegrini anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji majira haya ya joto
City imekuwa kwenye mazungumzo na
Fiorentina juu ya Jovetic kwa muda sasa, lakini inafahamika klabu hizo
mbili hatimaye zimekubaliana biashara hiyo kwa Pauni Milioni 23, ambayo
itapandisha kiwango cha malipo ya posho hadi Pauni Milioni 5.
Awali, ilivumishwa Fiorentina
hawatamuuza mwanasoka huyo wa kimataifa wa Montenegro, mwenye umri wa
miaka 23, kwa dau la chini ya Pauni Milioni 28.
City bado ina matumaini ya kumsaini
Negredo lakini inaonekana kushindwa kufika dau ambalo wanataka Sevilla,
Pauni zisizopungua Milioni 20.
Del Nido alithibitisha jana kwamba klabu
hizo mbilo zinapishana katia dau: "Aidha walipe tunachikitaka au
mchezaji abaki Sevilla kwa miaka mingine mitatu,".
Wakati huo huo, City imesema beki Aleksandar Kolarov hatajiunga na Juventus licha ya taarifa kwamba watasikiliza ofa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27
inaaminika anataka kuondoka, baada ya kupoteza nafasi yake katika beki
ya kushoto kwa Gael Clichy, lakini wakati Maicon akijiandaa kujiunga na
Roma kwa Pauni Milioni 4, City inataka kumbakiza Kolarov.

Anabaki tu: Manchester City inajiamini itambakiza Aleksandar Kolarov asiende Juventus

Ametoweka: Carlos Tevez tayari amehamia Italia
Kuondoka kwa Maicon ina maana
kutapunguza bajeti ya mishahara ya klabu hiyo kwa Pauni Milioni 40
majira haya ya joto kwani Mbrazil huyo alikuwa anachukua Pauni 100,000
kwa wiki Uwanja wa Etihad, wakati pia Kolo Toure, Wayne Bridge na Roque
Santa Cruz, nao wameondoka kama wachezaji huru.
Inakisiwa uhamisho wa Tevez Juventus
umeokoa kiasi cha Pauni Milioni 17 City katika bajeti ya mishahara na
posho huku klabu sasa ikitaka kufuata sheria ya matumizi mpya ya fedha
kiungwana.
Inaonekana hivyo kwa sababu Jovetic na
Negredo wataigharimu klabu hiyo Pauni Milioni 50 baada ya kumsajili kwa
Pauni Milioni 15, Jesus Navas na Pauni Milioni 30 kwa Fernandinho.
Mbrazil huyo aliichezea mechi ya kwanza City katika ziara ya Afrika
Kusini na ana matumaini ya kupata mafanikio chini ya Pellegrini licha ya
kipigo katika mechi ya kwanza.