KLABU ya Manchester United inajianda kuvunja rekodi yake ya usajili kwa kutuma ofa ya mwisho ya Pauni Milioni 35 kwa Barcelona ili kumsajili Cesc Fabregas.
Kiungo huyo wa Hispania ni mlengwa mkuu
wa David Moyes kocha huyo mkuu wa United akitazamiwa kuimarisha kikosi
chake kabla ya kuanza kwa msimu.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu England
wamekuwa kwenye majadiliano na Barcelona kwa wiki kadhaa, huku ofa za
awali za Pauni Milioni 26 na Milioni 30 zikipigwa chini na klabu hiyo ya
Katalunya
REKODI ZA USAJILI UNITED
Roy Keane (Nottingham Forest, £3.75m - Julai 1993)
Andy Cole (Newcastle, £7m - Januari 1995)
Jaap Stam (PSV, £10.75m - Julai 1998)
Dwight Yorke (Aston Villa, £12.6m - Agosti 1998)
Ruud van Nistelrooy (PSV, £19m - Julai 2001)
Juan Sebastian Veron (Lazio, £28.1m - Julai 2001)
Rio Ferdinand (Leeds, £30m - Julai 2002)
Dimitar Berbatov (Tottenham, £30.75m - Septemba 2008)

(£, maana yake Pauni)
Sasa, United inajiandaa kurejea na dau
la Pauni Milioni 35, ambalo litapiku dau la Pauni Milioni 30.75 ambazo
kocha Sir Alex Ferguson alitoa kumnunua Dimitar Berbatov mwaka 2008.
Hadharani, Barca wanaendelea kusistiza
Fabregas hatauzwa na kocha mpya Gerardo Martino amesema: "Siwezi
kujihusisha na akaundi za klabu, lakini kwa kuzingatia klabu
imekwishakataa ofa mbili, naweza kuhisi na ofa ya tatu nayo pia
itakataliwa,".
Tunafahamu
Fabregas amewaambia rafiki zake atafungua uwezekano wa kujiunga na
United na yuko tayari kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa
Arsenal, Robin van Persie.