WAKATI nyota wake wa kimataifa, Mganda Hamis Kiiza (Pichani), alitarajiwa kuwasili jana, uongozi wa Yanga umepanga kumbana awapatie barua ya klabu aliyokwenda kufanya majaribio nchini Serbia kabla ya kumpatia mkataba mpya.
Usajili wa Kiiza umegubikwa na utata kutokana na nyota huyo kuhitaji dau la sh mil. 45 huku uongozi ukitaka kumpa sh mil. 35 kwa mafungu, jambo ambalo linapingwa na nyota huyo.
Habari kutoka katika klabu hiyo zimedokeza kama mchezaji huyo atarejea na barua anaweza kusaini mkataba mpya wa sh mil. 35 na kwamba si zaidi ya kiasi hicho.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa Kiiza amekuwa akiwachanganya vichwa kwani amekuwa akihitaji mshahara si chini ya dola 1,000 na dola 2,000 za usajili kwa kila mwezi.