come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NEYMAR AMUITA ROONEY BARCA


Star man: Neymar played a key role as Brazil won the Confederations Cup
NYOTA wa Brazil, Neymar amemtaka mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kufikiria kuhamia Barcelona, akisema itakuwa ni ndito kucheza na mshambuliaji huyo wa England. 
Neymar, ambaye mwenyewe amejiunga na timu hiyo ya Katalunya mapema majira haya ya joto kwa dau la Pauni Milioni 48.6 kutoka Santos ya Brazil, ameitaja Camp Nou kama kituo sahihi kwa mchezaji mwenye kipaji kama Rooney. 
Nyota huyo wa Samba, aliyefunga bao tamu wakati Brazil ikiichapa 3-0 Hispania jana katika Fainali ya Kombe loa Mabara, amesema: "Mtindo wa soka tunaocheza (Barcelona) na viwango vya wachezaji tulionao- ni klabu sahihi kwa wachezaji wakubwa kujiunga nayo,". 
Nyota: Neymar alitoa mchango mkubwa kwa Brazil kutwaa Kombe la Mabara