come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Omollo taabani baada ya kichapo

Sammy Omollo

Siku za Sammy Omollo kama mkufunzi mkuu wa kilabu cha Ligi Kuu Kenya, Sony Sugar, zimehesabiwa baada ya timu hiyo kucharazwa 4-1 na waliokuwa wakivuta mkia Kakamega Homeboyz Jumapili iliyopita.

Mwenyekiti wa Sony aliyejawa na ghadhabu, Charles Odero alifoka kuwa usimamizi wa kilabu hicho umefika tama na matokeo duni na wanasaka atakayeshukua mahala pake kocha huyo wa zamani wa mabingwa Tusker FC.
“Nimekata tamaa na matokeo ya kocha Omollo. Kilabu kinachoshikilia mkia hakiwezi tuchapa hivyo.
“Tunafanya uamuzi kwani tunahisi Omollo hawezi mudu kazi hii licha ya kumpatia uhuru wa kusajili wachezaji anaotaka pamoja na kumpa usaidizi wote aliotaka. Nimezungumuza na makocha kadhaa ili kubainisha nani anaweza jukumu hili,” Odero aliambia supersport.com.
SuperSport.com wamebaini Sony wanafanya mazungumuzo na kocha wao wa zamani, Zedekiah ‘Zico’ Otieno aliyejiuzulu musimu uliopita kuwania kiti cha siasa lakini hakufanikiwa kuchaguliwa kama diwani.
Odero anasubiri Otieno kudhibitisha kama atachukua wathifa huo.